Rais William Ruto hivi leo ameongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu 11,692 wa NYS kule Gilgil kaunti ya Nakuru.

Akizungumza wakati wa hafla ya hiyo, Ruto amedokeza kuwa serikali inapania kuongeza idadi ya vijana wanaojiunga na NYS kutoka 10,000 hadi 20,000, kila mwaka kama njia ya kubuni nafasi za ajira kwa vijana.

Aidha ameziamuru wizara nne nchini kutenga angalau asilimia 30 ya nafasi za ajira vijana wa NYS.

Hali kadhalika amehimiza usimamaizi wa NYS kugeukia ukulima ili waweze kuimarisha uwezo wa kujitegemea kifedha.

March 3, 2023