Mahakama ya Narok imewapiga faini ya shilingi elfu 200 ,elfu 5 na elfu 100  ama kifungo cha mwaka moja gerezani wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kuuza nyama ya wanyamapori  katika kijiji cha mosiro Narok kaskasini.

Wawili hao james parsian kindi mwenye umri wa miaka 33 na john gori mwenye umri wa miaka 38 walikubali mashtaka matatu dhidi yao ikiwemo kuwinda wanyama pori bila ruhusa kutoka kwa shirika la kulinda wanyamapori nchini kws.

Hakimu Hezron Nyaberi aliwafahamisha kuwa wako  na siku kumi na nne za kukata rufaa ya hukumu iliyotolewa dhidi yao.

Kwa upande wake afisa wa KWS aliyekuwa akichunguza kesi hiyo Evans Kibet amesema kuwa hiyo itakuwa funzo kwa watu wanaowawinda wanyamapori kiholela huku akitoa wito kwa wakaazi kushirikiana na serikali kwa kuwashtaki wawindaji.

Share the love
October 24, 2023