Baadhi ya wakaazi wa Narok mjini wameibua hisia mesto kuhusu umuhimu wa ofisi ya mwakilishi wa kina mama katika kaunti. Kuna wale ambao wanasema kuwa ofisi hiyo haina umuhimu wowote na inastahili kutupiliwa mbali huku wengine wakihisi kwamba fedha zaidi zinastahili kutolewa ili kufanikisha miradi ya ofisi hiyo ya mwakilishi wa kina mama.
Hata hivyo, kuna wakaazi ambao kutoridhishwa kwao na baadhi ya viongozi waliowachagua ambapo wametilia shaka ofisi ya mwakilishi wa akina mama na naibu gavana.
Kulingana na wakaazi hao, majukumu mengi ya mwakilishi wa kina mama yanatekelezwa na mbunge huku majukumu ya naibu gavana yakitekelezwa na gavana.
Hali kadhalika wamehimiza viongozi hao haswa mwakilishi wa akina mama kutembelea maeneo tofauti kaunti ya Narok na kutoa ufadhili kwa vikundi za akina mama ili hao pia wahisi uwepo wake.