Papa Leo wa XIV hii leo aliongoza ibada ya misa ya shukrani iliyohuduriwa na makardinali walioshiriki uchaguzi pamoja na makardinali wengine walioko roma katika kanisa la Sistine chapel, akiwakumbusha kwamba wanapaswa kushikilia imani yao kwa Kristo huku akionya kwamba pale imani inapokosekana maisha hupoteza maana.

Hii ndio misa yake ya kwanza kama papa.

Katika mahubiri yake, Papa Leo alitoa wito wa kukuza uhusiano wa kibinafsi na Kristo kila wakati huku akisisitiza kwamba, bila imani, maisha hayana maana.Kando na hayo aliwatolea changamoto viongozi wa kanisa kuwa wanyenyekevu ili kumtukuza Kristo, akirejelea matamshi ya mtangulizi wake Papa Francis.

May 9, 2025

Leave a Comment