BY ISAYA BURUGU ,10TH DEC 2022-Utawala wa rais wa Marekani, Joe Biden umeituhukumu Urusi kutanua ushirikiano wake wa kijeshi na Iran kwa kuipatia Tehran mifumo ya kisasa ya ulinzi, helikopta na ndege za kivita.

Msemaji wa Baraza la Usalama wa taifa nchini Marekani, John Kirby ametoa madai hayo akiinukuu tathmini ya kijasusi iliyofanywa na Washington inayosema kwamba Urusi inaipatia Iran msaada wa kijeshi usio na mfano.

Amesema mahusiano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili yanaimarika ikiwemo mpango wa mataifa hayo kufungua kiwanda cha kuunganisha ndege zisizo na rubani nchini Urusi ambazo Iran imekuwa ikiipatia Moscow kuzitumia katika vita nchini Ukraine.

Hata hivyo, Urusi na Iran hazijatoa majibu kuhusiana na tuhuma hizo ambazo huenda zitaongeza shinikizo kwa jumuiya ya kimataifa la kuitikia wito wa Marekani wa kuitenga zaidi Urusi.

 

 

 

 

December 10, 2022