BY RADIO OSOTUA 9TH DEC 2022-Polisi wamewatia mbaroni vijana wawili wa makamo wakishukiwa kwa makosa ya kutumia nguvu kupita kiasi kutekeleza wizi wa simu.

Washukiwa hao Micheal Otieno mwenye umri wa miaka 28 na Festus Owiti mwenye umri wa miaka 30 walikamatwa jioni ya Desembe 7 eneol la Kayole hapa jijini Nairobi, kufuatia tukio hilo la wizi.

Walikamatwa baada ya mwanamke mmoja kupoteza simu pamoja na vitu vingine vya thamana.

Idara ya Upelelezi wa Jinai DCI ilisema, mmoja wa washukiwa alikamatwa akiwa kwenye duka la kutengeneza simu katika mtaa wa Obama. DCI walisema waliweza kunasa simu 50 zinazoshukiwa kua za wizi.

Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya tukio lingine kujiri baada ya mwanamume mmoja kuzuwiliwa kenye kituo cha polisi cha Kasarani baada ya kupatikana na simu 265 za wizi za aina ya Iphone.

Mwanamume huyo ambaye alikuwa wa miaka 29 pia alipatikana na simu 10 aina ya Android ambazo zilishukiwa kuwa za wizi.

Jamaa huyo alikamatwa na maafisa wa polisi baada ya upelelezi mkali kufanyika nyumbani kwa mshukiwa.

Ripoti ya jopo la upelelezi ilisema, “Simu hizo zinashukiwa kuibiwa kutoka kwa umma.”

Polisi waliendeleza uchunguzi kuwanasa jamaa wengine waliokuwa wakishirikiana na mshukiwa kuiba simu.

December 9, 2022