Mtumba

Waziri wa biashara uwekezaji na viwanda Moses Kuria amesema kuwa serikali inapania kuiondoa biashara ya Nguo Kuu kuu almaarufu “Mtumba” humu nchini, akisema kuwa hili litasaidia viwanda vya kutengeneza nguo nchini kujiinua na kuwaajiri wakenya wengi Zaidi.

Katika kikao na waandishi wa Habari mapema leo, Waziri kuria ameeleza kuwa sekta ya utengenezaji wa nguo nchini inafaa kuwaajiri watu wapatao milioni tano kama taifa la Bangladesh badala ya idadi ya sasa ya watu elfu 50 walioajiriwa katika sekta hiyo kwa sasa.

Aidha Waziri Kuria ameweka wazi kuwa serikali itatekeleza mipango hii baada ya mashauriano yanayofaa na vilevile kutafuta nafasi mbadala kwa wafanabiashara hawa kuku wakiweka mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa kipato cha wananchi hakijakatizwa.

November 1, 2022