BY ISAYA BURUGU,02,NOV,2022- Waziri wa utumishi wa umma Bi Aisha Jumwa anasema kuwa amejitolea kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanaboreshewa mazingira ya utenda kazi ili wajihisi weynye motisha.

Akizungumza lipozuru kituo cha huduma center jijini Mombasa,Waziri amesema kuwa kwa muda murefu watumishi wa umma wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu hali ambayo imechangia utenda kazi duni kwao.Pia Waziri amesema kuwa analenga kushinikiza kuongezwa kwa mishahara sawa na kuimarishwa kwa mazingira yao .

Kando na hayo Waziri anasema mikakati inafanywa kuongeza muda wa kufanya kazi kwa wafanyikazi wa vituo vya huduma kote nchini na haswa katika sehemu za mashinani ili wananchi kwenye sehemu hizo wapate kuhudumiwa vyema Zaidi.

Waziri pia amezuru kituo cha huduma kilichoko GPO Mombasa kuathmini hali ya utenda kazi.

 

 

 

November 2, 2022