BY ISAYA BURUGU,27TH OCT 2023-Zoezi la mwigo kwa minajili ya mtihani  wa kitaiafa kwa darasa la nane KCPE na tathmini ya KPSEA  inayotarajiwa kuanza jumatatu wiki ijayo limefanyika katika shule mbali mbali nchini leo.

Wanafunzi milioni 1.4 watafanya KCPE katika vituo 28,533 kote nchini. Wanafunzi milioni 1.28 nao watafanya tathimini ya KPSEA katika vituo 32,584.

Katika shule ya msingi ya Roots kaunti ya Nakuru hali ya imekuwa shwari huku zoezi hilo la mwisgo likiendeshwa vyema.Mwalimu mkuu wa shule hiyo Colins Odhiambo ameelezea  Imani kuwa mandalizi waliofanya yatawapa matokeo bora.

 Watainiwa wa KCPE mwaka huu ndio wa mwisho kabla ya mtaala wa elimu wa 8-4-4 kutamatika rasmi.

 

 

Share the love
October 27, 2023