BY ISAYA BURUGU,18TH JULY,2023-Huku mungano wa Azimio ukitarajiwa kurejelea mandamano yake kesho kuishinikiza serikali kushughulikia gharama ya juu ya kimaisha nchini,Wakazi wa Narok kaskazini wametakiwa kutoshiriki  mandamano  hayo.

Mbunge wa Narok kaskazini Agness Pareyio amewataka wafuasi wa mrengo huo wasalie  manyumbani ili kujiepushia  madhara  haswa baada ya majeruhi na vifo kuripotiwa sehemu mbali mbali  za nchi kufuatia mandamano hayo.

Pareyio amesema hatua hiyo imepelekea mali kuharibiwa sawa na kufuruga amani miongoni mwa jamii.Mbunge huyo wa chama cha Jubilee  amesema wakazi wa Narok kaskazini wanaunga mkono serikali kutekeleza kazi zake ipasavyo kushuhughulikia hali ya kiuchumi

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
July 18, 2023