BY ISAYA BURUGU,18TH JULY,2023-Tume ya huduma za mahakama imemteua Athman Abdulhalim Hussein kama chifu kadhi mkuu nchini.Hussein  ambaye ni kadhi zamani wa eneo la Nairobi atakuwa anachukua mahalama pa Ahmed Muhdha.

Uteuzi wake ulijiri baada ya tume hiyo kuendesha mahojiano ya wagombea waliorodheshwa  kwa wadhifa huo na ambao walikuwa wametuma maombi ya nafasi hiyo iliyotangazwa tarehe 14 mwezi April  mwaka huu  kabla ya jaji mkuu Martha Koome  jumatatu kutangaza kuwa JSC ilikuwa imemteua  Hussein.

Athman Abdulhalim Hussein Kadhi mkuu mpya-Picha Hisani

 

Wagombea waliokuwa wameorodheshwa na JSC  ni Pamoja na Sukyan Hassan Omar, Idris Nyamagosa Nyaboga, Athman Abdulhalim Hussein, Kutwaa Mohamed Abdalla na  Omari Hassan Kinyua walioshiriki kwenye mahojiano yaliyoendeshwa tarehe 22 mwezi Mei mwaka huu.

Mahakama za kadhi  zilibuniwa chini ya  kifungo 170 cha katiba ya Kenya  na zina jukumu la kushughulikia kesi  za ndoa za kislamu na Maisha ya familia kwa mjibu wa sharia  na pia kushugulikia maswala ya uridhi miongoni mwa waislamu.

 

Share the love
July 18, 2023