babu-owino-

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, ameachiliwa huru na mahakama kwa dhamana ya pesa taslimu ya shilingi laki moja au bondi ya shilingi laki mbili. Hii ni baada ya kufikishwa mahakamani kwa kesi inayomhusisha na kuongoza maandamano ya upinzani ambayo yalianza siku ya Jumatano wiki hii.

SOMA PIA : Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino Awasilishwa Mahakamani.

Washukiwa wengine sita waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo pia wameachiliwa kwa matakwa sawa baada ya kurejeshwa mahakamani asubuhi ya leo. Washukiwa hao ni pamoja na Calvina Okoth, anayejulikana kwa jina la Gaucho, Tom Ondongo, Michael Otieno, Pascal Ouma, Kevin Wambo, na Willys Owino. Wote wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika njama ya kuongoza shughuli za kuvuruga amani wakati wa maandamano ya upinzani.

Uamuzi wa kuwaachilia huru washtakiwa ulitolewa na Hakimu Mkuu Lukas Onyina, ambaye alieeleza kuwa upande wa mashtaka haukutoa sababu dhabiti za kuwanyima dhamana washukiwa hao.

 

 

 

July 21, 2023