BY ISAYA BURUGU 22ND JULY,2023-Mlinzi wa kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, Maurice Ogeta sasa ni mtu huru.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika chama cha ODM Philip Etale alithibitisha katika taarifa kwamba Ogeta aliachiliwa kutoka mikononi mwa polisi mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia Leo.

Etale alidai kuwa mlinzi huyo wa Odinga aliachwa katikati ya barabara ya Ruai na gari lake kuharibiwa.

Ogeta alikamatwa siku ya Jumatano kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya kuipinga serikali. Alikamatwa jijini Nairobi alipokuwa akiendesha gari kuelekea kazini asubuhi ya siku hiyo ya maandamano.

Afisa kutoka huduma ya polisi alithibitisha kuwa Ogeta alikuwa miongoni mwa wale waliolengwa kukamatwa na kuzuiliwa.

Kwa mjibu wa  afisa huyo alikuwa amefuatwa nyumbani kwake Langata.Kulingana na polisi, Ogeta alikuwa akizuiliwa katika seli za kituo cha polisi cha Utawala.

Kuachiliwa kwa Ogeta kulijiri baada ya mahakama kuamuru awasilishwe mbele ya mahakama yoyote nchini jana Ijumaa.Jaji Lawrence Mugambi alitoa uamuzi huo jana wakati kesi hiyo ilipowasilishwa mbele yake.

 

July 22, 2023