Wizara ya elimu imezindua mfumo mpya wa usajili wa wanafunzi KEMIS na kuondoa mfumo wa sasa NEMIS. Kwa mujibu wa katibu wa elimu Paul Bitok, mfumo huo utatekelezwa kwa awamu ambapo wanafunzi wataanza kusajiliwa kwa mfumo huo mpya mwezi ujao.

    Bitok amesema kuwa mfumo huo utatumika katika taasisi zote za elimu nchini kwa usajili wa wanafunzi.

    Ameongeza kuwa KEMIS itaimarisha Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu (NEMIS), ambao unakusanya data na taarifa kuhusu wanafunzi ili kufahamisha ugawaji wa rasilimali za elimu.

    May 15, 2025

    Leave a Reply