By Isaya  Burugu ,Oct 14,2022-Mlinzi  Mama Ida Odinga ameuuwa kwa kupigwa risasi.Afisa huyo wa polisi alipigwa risasi jana usiku katika mtaa wa Uzima huko Kisumu.

Jina la marehemu lilibanua hadi familia yake ifahamishwe kwanza kuhusu kifo chake.Mshukiwa ambaye anasemekana kuwa meneja wa mojawapo ya klabu maarufu mjini Kisumu alitoroka baada ya kupiga risasi afisa huyo.

Mshukiwa pia alimpiga risasi mwanamke aliyekuwa ameandamana na afisa huyo kwenye mkono. Mwanamume mwingine aliyekuwa na wawili hao pia alipigwa risasi mguuni.

Waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini wakiendelea kupokea matibabu.Kwa mujibu wa duru mbali mbali, mlinzi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kutofautiana na maeneja wa klabu moja mjini Kisumu.Mshukiwa ambaye anawindwa aliondoka na bunduki ya afisa aliyeuawa.

October 14, 2022