BY ISAYA BURUGU ,OCT 14,2022-Rais Wiliamu Ruto  hivi leo ameongoza hafla ya kuwakumbuka wanajeshi waliopoteza Maisha yao wakati wakilinda taifa hili katika nyakati tofauti.

Hafla hiyo imeandaliwa katika kambi ya kijeshi ya Laikipia Airbase.

Katika hafla hiyo rais amezindua sanamu iliyo na buti sawa na kofia kwa heshima ya maafisa wakijeshi walioaga dunia wakilinda nchi.

October 14, 2022