BY ISAYA BURUGU,1ST NOV,2023-Tume ya maadili na kupambana na ufisadi Eacc imemkamata mshukiwa wa utapeli ambaye amekuwa akijifanya mpelelezi mkuu mwenye mamlaka makubwa katika tume hiyo,huku akidaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na mkuruenzi mkuu wa tume hiyo Twalib Mbarak.

Shadrack Karira  Ndegwaanadaiwa kuwa amekuwa akidai kuwa na uwezo wa kufutilia mbali uchunguzi wa kesi za  ufisadi dhidi ya  mtu yeyote ama kuhujumu mkondo wa uchunguzi wa kesi za ufisadi dhidi ya watu wanaochunguzwa.

Pia amedaiwa kujidai kuwa mhudumu wa iara ya upelelezi wa jinai DCI au NIS.Mshukiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha EACC.

Kufutia kisa hicho,naibu mkurugenzi mkuu wa tume ya EACC Abdi Mahmud amewaonya wananchi na haswa maafisa wa umma kuwa wangalifu dhidi ya watu wanaojidai kuwa wafanyikazi wa tume hiyo ilhali lengo lao ni kuwahadaa.

 

 

 

November 1, 2023