BY ISAYA BURUGU 28TH DEC 2022-Mtu mmoja ameaga dunia leo  huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya modern coast  kuanguka mtoni kaunti ya Kisii.

Basi hilo liliripotiwa kupoteza mwelekeo  na kuacha barabara eneo la Masosa kabla ya kuanguka kwenye mto  Nyakomisaro  hivi leo asubuhi.

OCPD wa Kisii Central Amos Ambasa amedhibitisha kisa hicho  na kusem akuwa mtu mmoja aliifariki katika ajali hiyo  na ambaye alikuwa mtembeaji kwa miguu aliyegongwa na basi hilo baada yake kupoteza mwelekeo.

Amesema walionusurika wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kisii  ambapo wanaendelea kutibiwa.Basi hilo pia limeondolewa kutoka mtoni na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kisii.Mwili  wa aliyefariki umehamishiwa katika hifadhi ya miili ya hospitali ya rufaa ya Kisii.

 

December 28, 2022