BY ISAYA BURUGU ,28TH DEC 2022– Kamanda wa polisi kaunti ya Narok Kizito Mutoro amewataka Wenyeji wa Narok kuwa wangalifu kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushudiwa maeneo mbali mbali kaunti ya Narok. Kizito akizungumza ofisini mwake mjini Narok amesema mtu amesombwa na maji ya mafuriko kiza cha hivi punde ikiwa na ya mwanaboda boda mmoja ambaye amesombwa na maji eneo Trasmara magharibi katika mto Kongit  eneo la Olepolos Olchani Trasmara magharibi akijaribu kufuka mto kwa haraka. Katika kisa cha pili gari mbili aina ya Land Cruisers pamoja na Brobox yalisombwa na maji ya Mafuriko eneo Narok magharibi.

Wakati uo huo kamanda huyo wa polisi ametoa onyo hasa kwa madereva wanaokunywa pombe na kuendesha magari kuwa chuma chao ki motoni .Kizito amesema wakati wanajaribu kuendesha magari kwa mwendo wa kazi hatua ambayo imepelekea wengi kuaga dunia

December 28, 2022