BY ISAYA BURUGU 18TH AUG 2023-Mtu mmoja ambaye ni mwanafunzi ameaga dunia huku watu wengine 18 wakiachwa na majeraha baada ya kuhusika katika ajali ya bara barani eneo la Leperes kwenye bara bara kuu ya Narok-Bomet Narok.

Kamanda wa polisi Narok kusini Isaac Omari amesema kwamba ajali hiyo imehusisha matatu 2 moja kutoka kampuni ya South Rift na ingine kutoka kampuni ya Mizizi na yote yalikuwa yanatoka upande wa Bomet kuelekea Narok.

Omari anasema kwamba matatu kutoka kampuni ya Mizizi Sacco ilikuwa inajaribu kusimama kumchukua abiria mmoja aliyesimamisha gari hilo kubebwa lakini kabla ya kusimama akagongwa na matatu hiyo ingine ya South Rift kutoka nyuma hali iliyopelekea magari hayo mawili kuondoka bara barani na kuangukia ndani ya mtaro upande wa kushoto wa bara bara hiyo.

Hali hiyo ilipelekea mwanafunzi mmoja kufariki pindi tu alipowasilishwa katika hospitali kuu ya Ololulunga huku watu wengine 8 wakiachwa na majeraha mabaya na 10 wakaachwa na majeraha madogo.Miongoni mwa wale walioachwa na majeraha 6 ni wanafunzi.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Narok na hospitali kuu ya Ololulunga huku upasuaji ukitarajiwa kufanywa. Magari nayo yamepelekwa katika kituo cha polisi cha Ololulunga.

Share the love
August 8, 2023