BY ISAYA BURUGU 8TH AUG,2023-Halmashauri ya kitaifa ya kukabili pombe na mihadarati NACADA imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya ventanil ambaye inaminika kuibwa kutoka kwenye vituo vya afya na  na kusambazwa kwa umma eneo la pwani.

Kaimu mkurugenzi wa NACADA prof John Muteti anasema kuwa uchunguzi huo unaendeshwa na  washikadau mbali mbali husika ikiwemo bodi ya kudhibiti dawa na sumu huku vilevile NACADA ikiendelea kuzunguka kuchukua sampuli kutoka kwa wadhiriwa kabla ya kutoa ripoti kamili katika muda wa wiki mbili zijazo.

Haya yanajiri baada ya kanda za video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha watu waliolewa kupindukia kukiwa na madai kuwa walikuwa wamtumia dawa hiyo.

 

 

Share the love
August 8, 2023