Mwanamke ahumukiwa miaka 10

Mahakama ya Mombasa imemhukumu mwanamke mmoja kutoka eneo la Bombo, Kisauni katika kaunti ya hiyo, kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kuthibitika kuwa alimuua mwanawe wa mwaka mmoja kwa kumtupa kisimani. Mwanamke huyo, Happy Mwenda Mumba, alikuwa akipanga kusafiri kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu, na aliamua kutekeleza kitendo hicho cha kikatili ili apate fursa ya kusafiri bila mtoto.

Kesi hiyo iliyosikilizwa na Jaji Anne Ongtinjo wa Mahakama Kuu ya Mombasa ilifichua kuwa Mumba alitekeleza kitendo hicho cha kinyama mwezi Julai mwaka jana. Upande wa mashtaka ulithibitisha kwa ushahidi wa kutosha kuwa Mumba alihusika kwa makusudi katika kifo cha mwanae, na hivyo kuamua kumhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani.

Kulingana na uamuzi wa Mahakama, kitendo cha Mumba ni cha kusikitisha na kikatili, na kinakiuka maadili ya kibinadamu. Jaji Ongtinjo alisema kuwa uamuzi wa Mahakama unalenga kutoa onyo kwa wale wenye nia ya kutekeleza vitendo sawia vya kikatili.

 

Share the love
October 21, 2023