Kenya imeondoa mahitaji ya viza kwa raia wa Angola katika juhudi za kuimarisha biashara kati ya mataifa haya mawili. Rais Ruto alitoa tangazo hili leo wakati wa kikao cha pamoja na Rais wa Angola Joao Lourenco katika Ikulu jijini Nairobi.

Alisema hatua hiyo itarahisisha usafirishaji wa watu, bidhaa na huduma. Zaidi ya hayo, Rais aliahidi kuharakisha na kuhitimisha majadiliano ju ya kuanza tena kwa safari za ndege za moja kwa moja hadi Angola.Kenya na Angola zimetia saini mikataba 11 ya maelewano.

Aidha rais Ruto amemhakikishia rais Lourenco kuwa Kenya itaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuleta amani na utulivu nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Share the love
October 21, 2023