BY ISAYA BURUGU 11TH NOV,2022-Maafisa wa polisi kule Kisii wanachunguza kisa ambapo Mwanamume wa umri wa makamo kutoka Nyatieko, eneo la Kitutu Chache Kusini, kaunti  hiyo ya Kisii amemchinja mama yake baada ya kutofautiana kuhusu chakula.

Wanakijiji wa Bomiruga walisema mshambuliaji alitenda uhalifu huo usiku wa kuamkia leo  muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akiwa amechelewa.Polisi na wasimamizi wa mkoa wamesema Innocent Monyenye ,34, alikata mikono ya Kemunto Monyenye 74 vibaya baada ya kuchelewa kumpatia chakula.

Alifariki alipofika katika hospitali ya Kisii Teaching and Referral Hospital ambako alikimbizwa kwa matibabu.

Baadaye mshukiwa alikamatwa na umma na kusindikizwa hadi seli za polisi za Nyatieko.Mshukiwa, hata hivyo, alipata michubuko kichwani alipojaribu kutoroka kutoka kwa kundi la watu waliokuwa wakitaka kumwangamiza.

 

November 11, 2022