BY ISAYA BURUGU,11TH NOV,2022-Inspekta mkuu mpa wa polisi  Japheth Koome ameapishwa rasmi  kuanza jukumu lake.Hafla ya kuapishwa kwa Koome imeandaliwa katika  mahakama ya juu nchini na kuongozwa na jaji mkuu Martha Koome.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwake Koome ameapa kukabiliana na visa vinavyozidi kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Vilevile inspekta mkuu wa polisi ameweka wazi kuwa yeye hana uhusiano wowote wakifamilia na jaji mkuu Martha Koome tofauti na taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa katika mitandao yakijamii kuwa wawili hao wana uhusiano .

Koome anachukua rasmi wadhifa huo ambao umekuwa ukishikiliwa na Noor Gabow ambaye amekuwa kaimu inspeka mkuu wa polisi tangu mapema mwezi Agosti.

 

 

 

November 11, 2022