BY ISAYA BURUGU 13TH JAN 2023-Mwili wa mwalimu wa miaka 44 aliyeripotiwa kupotea tarehe 22 mwezi disemba mwaka jana umepatikana ndani ay sanduku nyumbani mwake katika Kijiji cha Ihururu kaunti ya Nyeri.
Mabaki ya Joseph Gathogo yamepatikana ndani ya chumba chake cha sebule baada ya harufu mbaya kuanz akutoka katika nyumba hiyo na kupelekea msimamizi wa nyumba Wiliam Gitau kuwapasha polisi Habari ambao walivunja nyumba ya marehemu.
Waligundua mwili wa mwalimu huyo wa shule ya sekondari ya Muhoya ukiwa umegongelewa misumari kwenye sanduku lililokuwa na muundo wa mashua lililokuwa kama kaburi.Shada la maua ,bendera nyeusi na mandishi yasiyosomeka yalipatikana na pembe vilipatikana kando ya mwili huo.
Kwa mjibu wa naibu chifu wa Muhoya Martha Wanjiru amesema siku ya kutoiweka kwake Mwlaimu huyo alikuwa ametoka kusimamia mtihani wa kidato cha nne KCSE uliyokuwa ukiendelea.Na hakuonekana tangu wakati huo.