Wahadhiri wa chuo kikuu cha Egerton kwa mara nyingine wamejitokeza kulalamikia mishahara yao ambayo hawajalipwa kwa miaka mitatu sasa.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wahadhiri hao wamewataka viongozi wa chuo hicho kufuata maagizo ya mahakama na kulipa mishahara yao asilimia bin mia.

Aidha wahadhiri hao wanamtaka naibu chansela wa chuo hicho prof. Isacc Kibwangi kujiuzulu kwa madai kuwa hawahusishi katika kutafuta suluhu ya kudumu.

January 13, 2023