Mwili wa Papa Francis ulihamishwa asubuhi ya leo kutoka Kanisa la Casa Santa Marta hadi Kanisa Kuu la St. Peter’s Basilica mjini Vatican, ambako waumini kutoka sehemu mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Mwili huo utasalia ndani ya basilika hiyo kwa muda wa siku tatu, na waumini wataruhusiwa kuendelea kumuaga kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliyeaga dunia Jumatatu, Aprili 21.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vatican, ibada rasmi ya mazishi itaandaliwa siku ya Jumamosi, ikiongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Mkuu wa Chuo cha Makardinali.

Baada ya misa ya mazishi, mwili wa Papa Francis utaelekezwa katika Kanisa Kuu la St. Mary Major Basilica, ambako utazikwa siku hiyohiyo ya Jumamosi.

April 23, 2025