Siku moja baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Meru kuandaa maandamano wakilalamikia hatua ya kupewa likizo ya lazima kwa naibu chansella wa chuo hicho Prof. Romanus Odhiambo, Waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu ameagiza kurejeshwa kazini mara moja kwa naibu huyo wa Chansella, na shughuli za kawaida kurejelewa mara moja.

Waziri machogu aidha ametaka usimamizi wa chuo hicho kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba hafla ya kufuzu kwa mahafali iliyoratibiwa kuandaliwa siku ya jumamosi inaendelea kama ilivyoratibiwa.

Wanafunzi chuoni humo walijitokeza kwa idadi zao kumpokea Naibu huyo wa Chansella alierejea ofisini hii alasiri ya leo.

March 7, 2023