Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amefanya mabadiliko chungu nzima katika wizara yake, baada ya kuwahamisha makamishena 20 hadi maeneo mbadala, na kuwapandisha cheo manaibu kamishena 12 hadi katika ngazi ya kuwa makamishena, huku makamishena 15 wakisalia katika vituo vyao vya sasa.

Baadhi ya waliopata uhamisho kuelekea maeneo mbadala ni Pamoja na kamishena wa kaunti ya Narok Isaac Masinde ambaye amehamishwa hadi katika kaunti ya  Homa Bay, huku mahala pake wapitarajiwa kuchukuliwa na David Kariuki Gitonga ambaye amepandishwa hadi kutoka kwa kuwa naibu wa kaunti kamishena.

Katika taarifa iliyochapiswa na Waziri Kindiki, makamishena wanne wamepata kurejeshwa katika makao makuu ya wizara hiyo, huku manaibu kamishena 8 wakipata uhamisho.

Share the love
March 7, 2023

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: