BY ISAYA BURUGU 11TH OCT 2023-Naibu Rais Rigathi Gachagua ameitaka jamii ya maa kujiepusha na mila potofu hasa ukeketaji, mimba na ndoa za mapema kwa mtoto wa kike. Gachagua akizungumza eneo la Kisherlmuruak Narok magharibi alipongoza hafla ya  ufunguzi wa bweni lililojengwa na fedha za hazina yaustawishaji wa maeneo  bunge CDF Narok magharibi amesema kuna haja ya jamii ya maa kukumbatia elimu kwa mtoto wa kike.

Gachagua ametoa wito kwa jamii ya maa kuipa kipaumbele maslahi ya wasichana kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto yao vile vile naibu rais amesema serikali imeweka mipango ya kuhakikisha kila mwanafunzi amepata elimu.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu ameahidi kushirikiana na serikali ya kitaifa kuimarisha miundo msingi kaunti ya Narok.

 

 

 

 

 

 

Share the love
October 11, 2023