Mamlaka ya kutwaa mali iliyopatikana kwa njia zilizo kinyume cha sheria (ARA) imetoa rai la kurejeshwa kwa shilingi milioni 200 zilizotwaliwa kutoka kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, ikisema kwamba fedha hizo zilipatikana kwa njia ya halali.

ARA sasa inaitaka mahakama ya rufaa nchini kutupilia mbali rufaa iliyoandikishwa na badala yake kuruhusu kurejeshwa kwa mali hiyo kwa Naibu wa rais.

Katika faili zilizowasilishwa mahakamani, afisa wa upelelezi katika mamlaka ya ARA, Sajenti Fredrick Musyoki, alieleza kuwa ARA haikufanya uchunguzi wowote wa madai ya DCI kwamba Bw. Gachagua alipata pesa hizo kwa njia ya ulaghai.

Musyoki ameongeza kuwa ARA ilitwaa mali ya Gachagua pasi na kukamilisha uchunguzi wowote, ila sasa iko tayari kurejesha mali hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wao.

January 2, 2023