Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amefanya mabadiliko katika idara hiyo, baada ya kuwateua waratibu/watawala wa mikoa wapya katika kanda zote nane humu nchini, pamoja na kufanya uteuzi wa maafisa katika wizara hiyo.

Kwa mujibu wa chapisho la wizara ya usalam wa ndani alasiri ya leo, Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa ni Pamoja na

  1. Rhoda Onyancha (Pwani)
  2. John Otieno (Kaskazini Mashariki)
  3. Paul Rotich (ukanda wa Mashariki)
  4. Fredrick Shisia (mkoa wa Kati)
  5. Flora Mworoa (Nyanza)
  6. Abdi Hassan (Bonde la Ufa)
  7. Samson Irungu (Magharibi)
  8. Katee Mwanza (Nairobi)

Wengine walionufaika na mageuzi haya ni Pamoja na Ann Ngetich ambaye ameteuliwa kutwaa wadhifa wa Katibu mkuu mratibu katika wizara ya usalama wa ndani, Beverly Opwora ambaye alikua Kamishena ya makueni ameteuliwa kuwa katibu wa utawala wa kitaifa, huku naye aliyekuwa kamishena wa kaunti ya Wajir Jacob Namule ametwaa wadhifa wa katibu wa maswala ya amani.

 

December 31, 2022