Radio Osotua › Local News

Naibu wa rais sasa adai viongozi wa azimio la umoja ndio walioitisha mazungumzo.

Local News April 6, 2023 Brigit Agwenge

Naibu wa rais Rigathi Gachagua sasa anadai kuwa viongozi wa muungano wa azimio la umoja ndio walioitisha mazungumzo na wala sio rais William Ruto.

Akizungumza katika kaunti ya Kiambu, Gachagua ameeleza kuwa hawatokubali masharti ambayo viongozi wa azimio wanatoa ndiposa mazungumzo yafanyike.

Aidha ametoa onyo kuwa iwapo viongozi hao watarejea kuandamana basi watakao patikana na kosa la kuharibu mali watachukuliwa hatua za kisheria.