President Ruto

Rais William Ruto amezindua mpango wa nyumba ya bei nafuu katika eneo la ongata rongai kaunti ya Kajiado adhuhuri ya leo, mpango unaopania kuwafaidi Zaidi ya wananchi 734 katika kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ruto amesema kuwa serikali yake inapania kupunguza bei ya vifaa vya ujenzi kwa minajili ya kushusha gharama ya ujenzi.Vilevile Ruto ameahidi kushirikiana na wamiliki wa ardhi binafsi ili kujenga nyumba zipatazo laki mbili za bei nafuu kwa wakenya kila mwaka.

Ruto aidha ametetea juhudi za serikali yake za kuhakikisha kuwa wakenya wanapata mikopo kwa ada ya chini, ili kujiimarisha kimaisha kupia kwa mikopo hii. Rais amesema kuwa serikali yake imeweka mipango kabambe ya kuwawezesha wananchi kupata mikopo kwa kiwango wanachoweza kulipa.

October 18, 2022