mshukiwa anaswa

Mwanaume mmoja wa umri wa makamo ametiwa mbaroni katika msitu wa Loita eneobunge la Narok kusini akihusishwa na hulka ya ukataji wa miti na uharibifu wa misitu. Akidhibitisha haya, naibu kamishana wa kaunti ndogo ya Narok kusini Bw. Felix Kisalu amesema mwanaume huyo aliyetambuliwa kama Wilson Keuwa, amekuwa mafichoni kwa wiki moja baada ya taarifa kuwa anawindwa na maafisa wa polisi.

Mbizo zake za sakafuni hata hivyo zilifikia ukiongoni siku ya Jumanne 18.10.2022, baada ya mafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi eneo la Entesikira kumtia mbaroni eneo la Olungarua baada ya wananchi kupiga ripoti kwa ofisi ya chifu eneo hilo.

Inadaiwa kuwa mshukiwa huyo alikuwa miongoni mwa washukiwa wengine wa kiume ambao wamekuwa wakitekelez aukataji wa miti. Pia wanadaiwa kuwajeruhi na kuwaacha na majeraha wazee wa kijiji pamoja na chifu wa eneo hilo walipojaribu kuwakamata huku wawili wao wakipoteza simu zao. Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi akisubiri kushtakiwa kwa kosa la uharibifu wa misitu na ukataji wa miti kinyume cha sheria.

October 18, 2022