Mahakama ya Nairobi imeagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kutoa ushahidi wote unaonuia kutumia katika kesi inayomkabili Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya.
Agizo hilo linakuja baada ya upande wa mashtaka kukiri kuwa umeshindwa kufuata amri ya awali ya mahakama iliyotaka kufichuliwa kwa nyenzo za kesi hiyo.Upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Victor Awiti, uliomba kuongezewa wiki mbili ili kutekeleza agizo hilo, akitaja changamoto za kupata hati kutoka kwa afisi za Kaunti ya Trans Nzoia.
Hata hivyo upande wa utetezi ulipinga vikali ombi hilo na kusema kuwa ni matumizi mabaya ya mchakato wa mahakama.
Katika uamuzi wake, mahakama iliamuru upande wa mashtaka ufichue nyenzo zote muhimu ifikapo Juni 16, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Gavana Natembeya anakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo upatikanaji wa mali ya umma kinyume cha sheria, mgongano wa maslahi na kunufaika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa fedha za umma.
Currently at the Milimani Law Courts for the mention of the EACC matter. pic.twitter.com/DKCrhuxCEc
— George Natembeya (@GeorgeNatembeya) June 3, 2025