Okiyah Omtatah

Seneta wa Busia Okiya Omtatah amewasilisha kesi mahakamani kupinga baadhi ya mapendekeo yaliyo katika mswada wa fedha wa mwaka 2023/24, akisema kwamba mswada huo ni kinyume cha Sheria.

Katika kesi hiyo iliyowasilishwa chini ya cheti cha dharura, Omtatah amesema kwamba baraza la mawaziri liliingilia majukumu ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini  KRA, pamoja na bunge la seneti na Bunge la Kitaifa. Seneta huyo ameeleza kwamba rais Ruto anapigia debe mswada huo, ambao utawalazimu wakenya kulipa ushuru bila mpango, na sasa anaitaka mahakama itoe agizo la kusimamisha mjadala huo na kumzuia Spika wa Bunge la Kitaifa kuwasilisha Mswada huo kwa Rais William Ruto.

Kuhusu mapendekezo ya ujenzi wa nyumba, Omtatah ameinyooshea serikali kidole cha lawama kw akupanga kukusanya fedha bila ya mwongozo wa bunge. Zaidi ya hayo amekosoa pendekezlo hilo akisema kwamba mswada wa fedha unafaa kushughulika tu na masuala ya fedha na wala sio miradi ya serikali.

 

Share the love
June 2, 2023