Muungano wa watengenezaji nchini KAM umeibua hisia kuhusu pendekezo la ushuru wa asilimia 3 wa ujenzi wa nyumba ambao unakuja wakati ambapo taifa linakumbwa na changamoto za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mkutano uliowaleta pamoja maafisa wa serikali, magavana pamoja na sekta ya kibinafsi, mwenyekiti wa muungano huo Rajan Shah alitaka kujua iwapo pendekezo hilo lina umuhimu kwa wakati huu ikizingatiwa kwamba biashara nyingi nchini zinapitia changamoto za kifedha kutokana na mfumko wa bei.

Watengenezaji hao pia waliitaka serikali kuwapa zabuni za kusambaza vifaa vya ujenzi iwapo pendekezo hilo litapitishwa.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na rais William Ruto.

June 3, 2023