Papa Leo wa XIV amemteua askofu Dominic Kimengich wa jimbo katoliki la Eldoret, kama askofu mkuu msaidizi wa jimbo kuu la Mombasa ambapo ana haki ya kumrithi askofu mkuu wa sasa.
Kama askofu mkuu msaidizi, mhashamu Kimengich atamsaidia askofu mkuu wa Mombasa katika usimamizi wa Idara ya kitume katika jimbo hilo. Uteuzi huo unahakikisha mwendelezo wa uongozi na kuimarisha misheni za kitume katika ukanda wa pwani.
Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB limekaribisha uteuzi huo na kuwahimiza waumini kumombea askofu Kimengich anapojitayarisha kuchukua wadhifa huo.

