BY ISAYA BURUGU 9TH OCT 2023-Mbunge mteule Sabina Chege hivi leo amepoteza wadhifa wake kama Naibu Kinara wa Wachache katika Bunge la Kitaifa.Kesi iliyowasilishwa na Chege katika Mahakama ya Kiambu kupinga uamuzi wa Azimio la Umoja wa kumwondoa katika wadhifa huo ilitupiliwa mbali na mahakama .

Kwa hivyo, Mbunge wa Embakasi Magharibi Mark Muriithi Mwenje anatazamiwa kuwa kinara mpya wa Wachache katika Bunge la 13.

Chama cha Jubilee  kimekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kisheria kuhusu uongozi, huku mrengo unaoongozwa na Chege ukipambana na mrengo unaoongozwa na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta kudhibiti chama.

Kenyatta amedokeza kuwa hatajiondoa katika chama hicho, akidumisha washirika wake katika nyadhifa kuu baada ya mzozo kati ya Chege na kundi la Kanini Kega, ambao wameamua kufanya kazi na Kenya Kwanza.

Share the love
October 9, 2023