BY ISAYA BURUGU,11TH NOV,2023-Maafisa wa polisi hapa mjini Narok,wameanzisha uchunguzi baada ya mtoto  mchanga wakiume wa siku moja kupatikanametupwa  katika shimo la choo nyuma ya bweni  kwenye chuo nani ya kikuu cha Masai Mara Karibu na mji wa Narok.

Kwa mjibu wa kamanda wa polisi wa Narok Kizito mtoro ,wanafuzni wa chuo hicho walisikia mtoto akilia ndani ya shimo hilo,na wakaripoti kwa maafisa wa polisi walio kwenye chuo hicho, na maafisa hao Pamoja na kundi ambalo hushughulikiwa majanga,

sawa   na   maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundu  walifika eneo hilo na kumuokoa huyo mtoto akiwa hai,na kumpeleka katika hospitali ya rufaa ya Narok ambapo anaendelea kutibiwa, huku hali yake ya kiafya ikiripotiwa kuwa nzuri.

Mwanamke aliyemtupa chooni mtoto huyo bado hajapatikana ijapokuwa polisi wanaendeleza uchunguzi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
November 11, 2023