BY ISAYA BURUGU,11TH NOV,2023-Wahudumu wa taxi kaunti ya Uasin Gishu wamelezea wasiwasi wao kuwa mpango wa serikali kuongeza bei ya mafuta kufikia shilingi mia tatu kwa lita utawatatiza pakubwa katika shughuli zao.

Wakizungumza na wandishi Habari mjini Eldoret,wahudumu hao wamesema tangu bei ya mafuta kuongezwa hadi Zaidi ya shilingi mia mbili kwa lita,wamekuwa wakihangaika huku biashara yao ikikosa kuwanufaisha na wakashangaa iwapo bei hiyo itapanda Zaidi hali kwao itawalemea na huenda wakalazimika kuachana na baishara hiyo.

Pia wamelezea masitikiko yao kuwa bei ya mafuta katika mataiafa mengine kama vile Tanzania ni ya chini na kuitaka serikali isake mbinu ya kukabili gharama ya juu ya mafuta.

 

 

 

 

Share the love
November 11, 2023