Raia wa Kenya wataruhusiwa kuingia katika mbuga za kitaifa na hifadhi za wanyamapori bila malipo Jumamosi hii wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Utalii.

    Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Septemba, na kaulimbiu ya mwaka huu, imejikita katika kuhakikisha Mabadiliko Endelevu katika sekta ya utalii duniani.

    Waziri wa utalii nchini Rebecca Miano, alisema mpango huu ni fursa kwa kila Mkenya kuweza kushuhudia urithi wa wanyamapori na umuhimu wao katika ikolojia ya Kenya.

    Kwa miongozo ya kuingia katika mbuga hizo bila malipo, umma umeombwa kutembelea tovuti ya KWS www.kws.go.ke au kufuatilia taarifa kwenye majukwaa yote rasmi ya mitandao ya kijamii ya KWS.

    September 23, 2025