Rais Mstaafu Uhuru Kenyattta ambaye anaongoza mchakato wa kutafuta amani kati ya serikali na waasi katika taifa ka kidemokrasia la Congo, amewataka wahusika kutoka pande zote kwenye mchakato huo, kuingia katika mazungumzo hayo wakiwa na moyo wa kupata suluhu, ili kuwezesha mchakato wenyewe kufanikiwa.

Kikao cha kujadiliana kuhusu kusitisha mapigano katika taifa hilo kimeandaliwa jijini Nairobi, pande zote husika Pamoja na washikadau wengine pia wakipata nafasi ya kuhudhuria.

Rais Mstaafu ameeleza imani yake kuwa mchakato huu utaleta faida chungu nzima kwa taifa hilo na hata kote ulimwenguni.

November 30, 2022