KAKAMEGA

Rais William Ruto ameandaa kikao cha Baraza la Mawaziri asubuhi ya leo katika ikulu ndogo ya Kakamega, huku akitarajiwa kukamilisha ziara yake katika ukanda wa magharibi mwa taifa.

Katika ratiba yake siku ya leo, rais pia ameratibiwa kuzindua ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneobunge la Vihiga, pamoja na kuzindua Kituo cha CT Scan katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Vihiga.

Vilevile rais ameratibiwa kukutana na wananchi katika Kituo cha kibiashara cha Shamakhokho, kabla ya kuihitimisha ziara yake kwa Kuzindua ujenzi wa Barabara ya Mago-Mululu-Lusui, katika eneobunge la Sabatia. Ziara ya Rais ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa taifa, ililenga kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, huduma za afya, na miundombinu ya usafiri katika eneo hilo.

Share the love
August 29, 2023