BY ISAYA BURUGU,7TH AUG 2023-Ziara ya rais Wiliam Ruto eneo la kati mwa nchi imeingia siku ya tatu hivi leo.Akikutana  na wenyeji wa kaunti ya Nyeri hivi leo,rais aliandamana na viongozi wengine wakuu serikalini.rais Wiliam Ruto ameanzisha muradi wa ujenzi wa Barabara ya  Ijiara inayoelekea ruteni eneo bunge la Mukurweini.Baadaye waliendelea na ziara yao huku wakizindua miradi mbali mbali wakimaendeleo eneo hilo.

. Rais pia alifuliliza moja kwa moja hadi Othaya ambapo alizindua muradi wa Maji na pia alifika eneo bunge la Tetu ambapo alizindua muradi wa maji.Rais na ujumbe wake pia walifika eneo bunge la Nyei mjini ambapo alizindua kituo cha kuegesha magari mjini Nyeri.Rais ameguzia swala la mazunguzo ya mariadhiano kati ya Viongozi wa mungano wa Azimio la umoja na wale wa Kenya Kwanza ambapo rais amesema kuwa ni sharti viongozi wa Azimio watangaze kuwa hapatakuwa ten ana mandamano ya uharibifu wa mali na amani nchini.

 

 

 

August 7, 2023