Rais William Ruto alasiri la leo ameongoza shughuli za kuweka msingi kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mfumo wa usafiri wa reli katika jiji la Nairobi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika kituo kikuu cha reli jijini Nairobi, rais amesema kukamilika kwa mpango huu kutainua hadhi ya jiji la Nairobi, na kupunguza msongamano wa magari jijini Nairobi.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Pamoja na naibu wa Rais Rigathi Gachagua, Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen na gavana wa Nairobi Johnson Sakaja.

December 7, 2022