Viongozi wa upinzani chini ya Muungano wa Azimio la Umoja wametoa orodha ya matakwa 12 wanayotaka yashughulikiwe na serikali ili kuyaboresha Maisha ya wananchi.

Viongozi hao wkiongozwa na Raila Odinga, Martha Karua na Kalonzo Musyoka, walitoa makataa yao baada ya kuandaa kikao cha mashauriano katika uga wa Kamukunji, adhuhuri ya leo, kwa nia ya kusikiliza maoni ya wakenya kuhusu mkondo ambao taifa linafuata.

Baadhi ya makataa yaliyotolewa na viongozi hao ni Pamoja na kurejeshwa kwa rezuku iliyokuwako kwa bidhaa muhimu kama vile unga, umeme na hata karo ifikiapo mwezi Januari mwaka ujao, kurejeshwa kwa mpango wa kuwasaidia wazee na wasiojiweza katika jamii Pamoja na kufuatwa kwa katiba katika mchakato wa kuwaondoa makamishena wa tume huru kama vile tume ya IEBC.

Pia wameitaka serikali kuurejesha mpango wa kutoa ajira kwa Vijana wa Kazi Mtaani, kurejesha marufuku iliyokuwapo dhidi ya vyakula vya GMO miongoni mwa matakwa mengine.

December 7, 2022