Rais Ruto

Rais William Ruto ameanza ziara ya siku mbili katika taifa la India, baada ya kukamilika kwa kwa ziara yake kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 nchini Dubai.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na msemaji wa ikulu Hussein Mohammed, Kiongozi wa taifa anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, mazungumzo yatakayozunguka masuala ya kilimo, biashara, kukuza uwekezaji, na ushirikiano wa huduma za afya miongoni mwa sekta nyingine muhimu ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa dawa.

Rais Ruto pia atakutana na Rais Droupadi Murmu katika ziara yake kwenye taifa hilo.

December 4, 2023